Kifo na yaliypo baada yake katika Uislamu

7.96 MB 89 1 Files
albyan
or download free
[free_download_btn]

Description

"Kila nafsi itaonja mauti." [Qur'an 29:57]

Mauti iko Karibu

"Popote mtakapokuwa, mauti yatawakuta hata kama mtakuwa katika ngome zilizojengwa imara na za juu!" [Qur'an 4:78]

Mauti ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuukimbia. Inakaribia kila siku; kila saa; kila dakika. Kulingana na CIA’s The World Factbook 2007, karibu watu wawili hufa kila sekunde. Hilo ni jambo la kushangaza: watu milioni 57.9 kila mwaka! Kila kiumbe atafikia hatima hii isiyoweza kuepukwa, bila kujali umri wake, afya, historia, hadhi ya kijamii au uchamungu wake au Imani yake. Wako wapi wafalme wa zamani, matajiri na wenye nguvu? Wako wapi waliokuwa wazuri, maarufu, na wasomi wa kiakili?

Ukweli wa Mauti

Kifo si janga, bali ni mpito kutoka dunia hii hadi akhera. Inapaswa kutufanya tufikirie na kutafakari kuhusu lengo la maisha, na nini kitakachotokea kwetu baada ya mauti.

Allah ametujulisha katika Qur’an kwamba Ametuumba kwa kusudi la kumuabudu Yeye peke Yake na kwamba maisha haya ni mtihani kuona nani atatimiza lengo hilo:

"Sikuwamuumba majini na wanadamu isipokuwa kwa ajili ya kuniabudu." [Qur’an 51:56]

Mwenyezi Mungu pia ametufahamisha kuhusu kusudi la kuumba mauti na uhai:

"Yeye ndiye Aliyeumba mauti na uhai ili Awajaribu nani kati yenu atakuwa bora kwa matendo." [Qur’an 67:2]

Mtu haandalii mauti kwa kulipia huduma za mazishi mapema au kuchagua jeneza kabla ya wakati. Bali inahusiana na kutimiza lengo la maisha – kumuabudu Allah pekee, kuishi kulingana na amri Zake, na kufanya matendo mema. Dhana ya ibada katika Uislamu ni ya kina na haihusishi kuswali tu. Kwa kweli, kitendo chochote kinachomfurahisha Allah kinahesabiwa kuwa ibada, na mtu atalipwa mema kwa hilo.

Wakati wa kifo

"Kila nafsi ifikirie yale iliyotanguliza kwa ajili ya kesho." [Qur'an 59:18]

Kila siku tunaona mifano ya mauti. Tunaona kifo cha amani kama kile kisicho na maumivu au vurugu. Hata hivyo, si lazima iwe hivyo. Wakati mtu anapokufa, roho hutoka mwilini, na hivyo mwonekano wa mwili hauwezi kuonyesha hali ya roho. Utulivu au wasiwasi wa roho utatokana moja kwa moja na jinsi mtu alivyoitimiza kusudi lake katika maisha haya, na haihusiani na sababu ya kifo.

Fikiria mfano wa watu wawili wenye tiketi ya safari ya njia moja kwenda mahali ambapo hawajawahi kufika. Mtu wa kwanza anatumia muda kujifunza lugha, utamaduni, na mazoea yanayohusiana na safari yake. Anapata sarafu sahihi na chanjo zinazohitajika, na wakati wa kusafiri ukifika, anawasili bila mshangao wowote. Yuko salama na ameridhika kwa sababu alichukua muda kujiandaa.

Kwa upande mwingine, mtu wa pili hajajiandaa vizuri na anaishi tu kwa muda hadi wakati wa kuondoka ufike. Anawasili mahali pasipojulikana akiwa na hofu na kuchanganyikiwa.

Kutokuwa tayari kwake kunasababisha apate hatima mbaya, kwa sababu vitu vyote alivyobeba havina faida yoyote.

Allah anasema katika Qur’an Akielezea mtu asiyejali kama huyu,:

"Mpaka mauti yanapomfikia mmoja wao husema, ‘Mola wangu nirudishe ili nifanye mema niliyoyaacha!’ Sivyo hivyo! Haya ni maneno tu anayoyasema." [Qur'an 23:99-100]

Fikiria pia jibu la wale waliotupwa Motoni, wanapoulizwa kuhusu kilichowafikisha huko:

"Watasema, ‘Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali, wala hatukuwalisha masikini, na tulikuwa tunazama katika upuuzi pamoja na wale waliokuwa wakizama, na tulikuwa tukikanusha Siku ya Malipo mpaka mauti ya hakika yalipotufikia.’" [Qur’an 74:43-47]

Sote tuna wakati wa kufa uliopangwa, na tutasafiri hadi mahali pasipojulikana. Jiulize - Je, umejiandaa kwa hilo?

Kusudi la Maisha

"Je, mlidhani kwamba Sisi (Mungu) tuliwaumba kwa mchezo (bila kusudi), na kwamba hamtarudishwa Kwetu?" [Qur’an 23:115]

Maisha ni mtihani unaomalizika kwa mauti, lakini hauashirii mwisho wa uwepo wa mtu.

Mara tu mauti inapofika, nafasi ya kufanya mema huisha. Itakuwa umechelewa kutubu na hatima yetu itaamuliwa tu kwa imani na matendo tunayofanya katika maisha yetu ya sasa.

Maisha ya mwanadamu yamegawanywa katika sehemu mbili: muda mfupi hapa duniani, na maisha ya milele katika Akhera. Akili yoyote yenye busara itaona kuwa furaha ya milele ni bora zaidi kuliko raha za muda mfupi duniani.

Allah alimuumba mwanadamu na kutufanya tuwajibike kwa matendo yetu kwa kutupatia uhuru wa kuchagua na akili ya kutambua jema na baya. Kama kusingekuwa na Akhera ambapo wema wanapata thawabu na waovu wanapata adhabu, hilo lingepingana na uadilifu kamilifu wa Allah.

Kwa hivyo ni uaadilifu wa kweli kwamba kuwe na Siku ya Kiyama ambapo kila nafsi itahukumiwa.

"Je, tutawafanya Wenye Imani kuwa sawa na Wakosefu? Mna nini? Mnahukumu vipi?" [Qur'an 68:35-36]

Siku ya Kiyama

" Sema hakika Mauti mnayoyakimbia yatakufikieni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri (yaani Allah) na Atakujulisheni mliyoyatenda." [Qur’an 62:8]

Matendo yote ya kila mtu katika maisha haya yameandikwa na kuhifadhiwa kwa umakini, kama Allah Anavyosema:

"Na kitabu (cha matendo) kitawekwa wazi, na utawaona wakosefu wakiwa na hofu kubwa kwa yale yaliyomo ndani yake." "Watasema, ‘Ole wetu! Kitabu hiki hakiachi chochote kidogo wala kikubwa bila kukihesabu!’" "Na watakuta yote waliyoyatenda yakiwa mbele yao." "Na Mola wako hamdhulumu yeyote." [Qur’an 18:49]

Tutashangazwa na usahihi wa rekodi kama hiyo ya matendo yetu yote, kwani tutakumbushwa mambo ambayo tuliyasahau zamani. Allah Anasema,

"Allah Amehesabu hayo, nao wamesahau." [Qur’an 58:6]

Kufikiria kwa kina jambo hili kunapaswa kutufanya tuone aibu kutenda dhambi yoyote tukijua kwamba itarekodiwa dhidi yetu na kufichuliwa Siku ya Kiyama mbele ya Allah.

Kwa wale wanaotia shaka uwezo wa Allah wa kufufua na kuwahukumu, Allah ananukuu maneno ya makafiri:

"Watasema, ‘Nani atayefufua mifupa hii wakati imeshakuwa mavumbi?’" "Sema (Ewe Muhammad), ‘Atayafufua Yule Aliyeumba mara ya kwanza! Na Yeye ni Mwenye kujua kila kiumbe.’" [Qur’an 36:78-79]

Peponi na Motoni

Wale wanaomuamini Allah kama Mungu pekee anayestahili kuabudiwa, na wanaofanya matendo mema, watapewa Pepo.

"Hakika watu wa Peponi siku hiyo watakuwa wakifurahia mambo ya kufurahisha." "Wao na wake zao watakuwa katika vivuli vizuri, wakiwa wameegemea juu ya viti vya enzi." "Watakuwa na matunda (ya kila aina) ndani yake, na watapata wanachokitaka." [Qur'an 36:55-57]

Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie) alisimulia kwamba Allah alisema:

"Nimewaandalia waja Wangu wema mambo mazuri ambayo jicho halijawahi kuona, sikio halijawahi kusikia, wala hayajawahi kufikirika moyoni mwa mwanadamu."

Hii ni tofauti kabisa na watu wanaokanusha Upweke wa Allah, ambao wataambiwa:

"Hii ndiyo Jahannam mliyokuwa mkiahidiwa!" "Chomeni humo leo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru." [Qur'an 36:63-64]

Kwa makafiri kuna adhabu kali zaidi:

"Hakika Jahannamu inangojea kwa waliyo asi ndio makaazi yao, ambapo watakaa humo karne baada ya karne." "Hawatapata humo baridi wala kinywaji chochote isipokuwa maji yanayochemka na usaha wa vidonda - malipo sawa na matendo yao maovu!" "Hakika hawakutarajia hesabu yoyote, na walizikanusha aya zetu kwa ukali kabisa." "Lakini kila kitu tumekiandika katika Kitabu." "Basi onjeni adhabu hii, na hatutawaongezea ila mateso zaidi." [Qur’an 78:21-30]

Hitimisho

"Ewe mwanadamu! Ni kitu gani kilichokudanganya juu ya Mola wako Mkarimu?" "Aliyekuumba, Akakutengeneza kwa uzuri na Akakupa kipimo kinachostahiki." "Katika sura yoyote Aliyopenda, Amekuweka pamoja." "Sivyo! Bali mnakadhibisha Malipo (Siku ya Kiyama)." [Qur'an 82:6-9]

"Hakika wema watakuwa katika neema, na hakika waovu watakuwa katika Moto." [Qur'an 82:13-14]

Kifo hakiepukiki. Lengo letu maishani ni kumuabudu Allah pekee, kufanya matendo mema na kuepuka yote yaliyokatazwa. Hatima yetu inaamuliwa kwa matendo yetu ya sasa, kwa hivyo tunaweza kutumia fursa zetu duniani kuhakikisha mahali pa milele Peponi, au tunaweza kuyapoteza na kujihukumu kwa adhabu ya milele Motoni.

Similar Downloads

No related download found!