Description
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Uislamu ni nini na Waislamu ni akina nani?
Uislamu ni mfumo wa asili na kamili wa maisha unaohimiza mtu kuzingatia uhusiano wake na Allah na viumbe Wake. Inafundisha kwamba roho hupata furaha na utulivu wa kweli kwa kutenda matendo mema ambayo Allah anayakubali ambayo yananufaisha jamii na mtu binafsi.
Ujumbe wa Uislamu ni rahisi: ni kumuamini na kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja wa Kweli pekee, na kumkubali Mtume Muhammad (rehma na amani zimshukie) kama Mjumbe Wake wa mwisho. Neno "Uislamu" lina maana ya kujisalimisha kwa Allah, na wafuasi wake wanajulikana kama Waislamu, ambao wanaweza kutoka katika asili au kabila lolote.
Nini lengo la Maisha?
Mungu hakuumba wanadamu ili wazurure bila malengo. Badala yake, tuna lengo la juu zaidi - kumtambua na kumuabudu Allah pekee, ili tuishi kwa mwongozo wa Muumba wetu. Mwongozo huu hutuwezesha kuishi maisha yenye mafanikio na baraka katika nyanja zote, katika dunia hii na Akhera. Mtihani wa imani ni kutumia akili na uwezo wa kufikiria kutafakari na kutambua ishara za Allah na kuishi kwa mujibu wa mwongozo Wake.
Kwa hekima Yake kuu, Allah aliwapa wanadamu uhuru wa kuchagua kama mtihani kuona nani atakayefuata njia Yake kwa hiari.
Allah ni nani?
Allah ni jina la kibinafsi la Mungu Mmoja wa Kweli. Allah hana mshirika, mfano, wazazi wala watoto. Sifa zote za Allah ni za ukamilifu, kama vile Muumba, Mwenye Rehema, Mwenye Nguvu, Mwenye Haki, mwadilifu na Mwenye ujuzi. Hakuna binadamu au kitu chochote kinachoshiriki katika utawala wa Allah au sifa Zake za Uungu, kwa hivyo, Yeye pekee ndiye anayestahili kuabudiwa moja kwa moja na kwa upekee.
Muhammad ni nani?
Muhammad (rehma na amani zimshukie) ni Mtume wa mwisho katika mfululizo ndefu ya Manabii, aliyetumwa kuwaita wanadamu wote kumuabudu Allah pekee. Alikuwa baba bora, mume, mwalimu, kiongozi na hakimu, na mfano kamilifu wa binadamu mwaminifu, mwadilifu,mkweli mwenye huruma na shujaa. Ingawa anaheshimiwa sana, kama Manabii wengine, na hakuabudiwa na Waislamu.
Kwa nini tunaamini Mwenyezi Mungu?
Kuna sababu nyingi za kumuamini Mungu, ikiwemo zile zinazotokana na mantiki rahisi (zilizofupishwa hapa chini) na kupitia ufunuo (utakaotajwa katika sehemu inayofuata).
- Mwanzo wa Ulimwengu - Sababu rahisi ya kumuamini Mwenyezi Mungu inahusiana na kutafakari asili ya ulimwengu. Je,kwa ufupi ulimwengu ulitoka wapi? Ulimwengu haujakuwepo daima (una mwanzo kulingana na sayansi ya kisasa) na hauwezi kuwa umetokea bure au kujiumba wenyewe. zingatio la busara ni kwamba liliumbwa. Tofauti na ulimwengu, Muumba wa ulimwengu, Mungu, ni wa milele, hana mwanzo na amekuwepo daima.
- Utaratibu wa Ulimwengu - Sababu nyingine rahisi ya kumuamini Mwenyezi Mungu ni kutafakari utaratibu wa ulimwengu kwa kutumia mantiki ifuatayo:
1. Chochote kilicho na mpangilio kinaonyesha uwepo wa akili
2. Mfumo wetu wa jua una mpangilio wa hali ya juu na sheria, mifumo na michoro changamani
3. Kwa hivyo, mpangilio katika ulimwengu wetu unaonyesha uwepo na akili ya Muumba
Qur'an ni nini?
Qur'an ni maneno halisi la Mwenyezi Mungu na ufunuo wa mwisho kwa wanadamu.
Qur'an inatoa hoja madhubuti kuhusu uwepo wa Mwenyezi Mungu kwa wale walio na nia safi na ukweli. Hauwezi kulinganishwa katika mtindo wake, hekima, mwongozo, uzuri na ufasaha wake. Ni maneno la Mwenyezi Mungu kama lilivyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (rehma na amani zimshukie) kupitia Malaika Jibril, na linapitiliza mafundisho yote ya awali, kama vile Injili na Taurati. Ni chanzo kikuu cha maarifa ya Kiislamu. Inafafanua na kueleza masuala mengi kama vile lengo la kuwepo kwetu; dhana sahihi ya Mwenyezi Mungu; matendo anayoyapenda na kuyachukia Mwenyezi Mungu; hadithi za Manabii na mafundisho; maelezo kuhusu Pepo, Moto na Siku ya Kiyama. Mojawapo ya miujiza mikuu ya Qur'an ni kwamba imesalia salama na haijabadilika tangu ilipoteremshwa zaidi ya miaka 1400 iliyopita. Ina pia mambo ina ukweli mwengi wa kisayansi na kihistoria ambayo hayakujulikana wakati huo na yamegunduliwa hivi karibuni tu, ambayo ni moja ya ushahidi kwamba Qur'an imetoka kwa Mwenyezi Mungu.
Ni zipi Ibada Kuu katika Uislamu?
Nguzo ya kwanza: Shahada. kushuhudia kuwa hakuna mungu anayestahili kuabudiwa isipokuwa Allah, na Muhammad ni Mtume Wake Allah.
Nguzo ya pili: Swala. Kuswali mara tano kila siku: alfajiri, adhuhuri, alasiri, magharibi, na isha.
Nguzo ya tatu: Zaka – Hii ni sadaka ya lazima inayotolewa kila mwaka kwa wasiojiweza, ikiwa ni sehemu ndogo (2.5%) ya jumla ya akiba ya kila mwaka.
Nguzo ya nne: Kufunga Mwezi wa Ramadhani. Katika mwezi huu, Waislamu wanajizuia kula, kunywa na mahusiano ya ndoa kuanzia muda wa alfajiri hadi jua kuzama
Ibada ya tano: Hija. Kila Muislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda kuhiji Makka angalau mara moja katika maisha yake.
Waislamu Wanaamini Nini Kuhusu Yesu na Manabii Wengine?
maelfu ya Manabii walitumwa na Allah, angalau mmoja kwa kila taifa, na ujumbe uleule: kumuabudu Allah peke yake na kutomshirikisha na yeyote. Baadhi ya hawa Manabii ni Adam, Nuhu, Yusufu, Ibrahimu, Yakobo, Isaka, Musa, Yesu na Muhammad (amani iwe juu yao wote).
Yesu alizaliwa kimuujiza bila baba na alifanya miujiza mingi – yote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Yesu (amani iwe juu yake) alikuwa mmoja wa Manabii wakubwa waliotumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu.
Yesu si Mungu wala mwana wa Mungu wala sehemu ya Utatu, kwani hili linapingana wazi na mafundisho safi ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu. Fikiria yafuatayo:
· Kuna mifano mingi katika mafundisho ya Kikristo ambapo Yesu anazungumza na kutenda kama kwamba Mwenyezi Mungu ni tofauti naye, kwa mfano, Yesu anaposwali kwa Mwenyezi Mungu – ikiwa Yesu alikuwa Mungu, alikuwa anaswali kwa nani?
· dhana "Mwana wa Mungu" linatumiwa kwa njia ya ishara katika lugha za awali za Biblia kumaanisha "mtu mwema" kwa watu wengi - si kwa Yesu pekee. Tatizo linatokea pale neno hili linapotumiwa kihalisi au kwa njia nyinginezo.
Ingawa Waislamu wanampenda na kumheshimu Yesu (na Manabii wengine wote), hawamuabudu wala kumpa sifa za Uungu, kwani sifa hizi ni za Mwenyezi Mungu pekee.
Je, Dini zinafanana?
Ingawa dini nyingi zina mafundisho sawa kuhusu tabia njema na kuwatendea wema wengine, Uislamu pia unazingatia sana ukubwa wa Mwenyezi Mungu bila kufanya maafikiano juu ya Upweke na Ukamilifu Wake. Tofauti na dini nyingine, Uislamu unafundisha kwamba Mwenyezi Mungu ni tofauti kabisa na wa kipekee akilinganishwa na viumbe Vyake na kwamba sifa zote njema na ibada zinapaswa kuelekezwa moja kwa moja na kwa upekee Kwake. Uislamu pia ni wa kina; rahisi lakini wa kina; na una ufunuo ulihifadhiwa; haukatai Manabii wowote wa Mwenyezi Mungu bali unakiri kwamba wote walikuja na ujumbe uleule.
Nini Hutokea Baada ya Kifo?
Kifo ni kuhamia kutoka maisha haya mafupi kwenda kwenye maisha ya milele yajayo.
Kila mtu atafufuliwa ili ahesabiwe Siku ya Kiyama. Mtu akiishi maisha mema na yenye heshima kwa kumuabudu na kumtii Allah, ataingizwa Peponi kwa Rehema ya Allah. Wakichagua ushirikina, basi Moto wa Jahannam unawasubiri.
Kama hakuna maisha baada ya kifo ambapo wema wanazawadiwa na waovu wanaadhibiwa, hilo lingepingana na haki kamilifu ya Mwenyezi Mungu, na maisha hayangekuwa ya uaadilifu.
- Uislamu Unawaonaje Wanawake?
Katika Uislamu, wanaume na wanawake wanachukuliwa kuwa sawa mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa kupokea thawabu na kuhesabiwa kwa matendo yao. Mwenyezi Mungu, Muumba wa jinsia zote mbili, amewapa kila mmoja majukumu tofauti, akizingatia tofauti zao. Wanawake wanapewa heshima kubwa na ukarimu, na hakuna aina yoyote ya dhulma inayoruhusiwa dhidi yao.
Je, Dhana ya Dhambi ya Asili Ipo Katika Uislamu?
Dhana ya "dhambi ya asili" haipo katika Uislamu. Mwenyezi Mungu ni mwadilifu; hakuna mtu anayewajibishwa kwa dhambi ambayo yeye mwenyewe hajaifanya.
Jihad ni nini?
Kiini cha Jihad ni kujitahidi na kujitolea kwa ajili ya dini kwa njia inayompendeza Mwenyezi Mungu. Kiisimu, inamaanisha "kujitahidi" na inaweza kumaanisha kujitahidi kufanya matendo mema, kutoa sadaka, au kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Aina inayojulikana zaidi ni Jihad ya kijeshi ambayo inaruhusiwa ili kuhifadhi ustawi wa jamii, kuzuia dhulma, na kuendeleza uadilifu.
Je, Uislamu Unaruhusu Ugaidi?
Katika vita, kushambulia raia wasio na hatia ni kitendo cha kuchukiza ambacho Uislamu unakikataza waziwazi. Kwa hakika, Waislamu hawaruhusiwi kuharibu mimea na wanyama bila ya kuwa na dharura, pamoja na wanadamu wasio na hatia. Hii ni mfano mmoja tu kati ya misingi ya kimaadili ya vita iliyoainishwa katika Uislamu. Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha kati ya ugaidi na upinzani halali dhidi ya uvamizi, kwa kuwa ni mambo mawili tofauti kabisa.
Chakula Halali ni nini?
Chakula halali, au kinachoruhusiwa, ni kile kilichoruhusiwa na Mungu kwa Waislamu kula. Kwa ujumla, vyakula na vinywaji vingi huchukuliwa kuwa halali, isipokuwa nguruwe na pombe. Nyama na kuku lazima zichinjwe kwa njia ya kibinadamu na sahihi, ikiwemo kutaja jina la Mungu kabla ya kuchinja na kupunguza mateso ya wanyama.
Nani Anaweza Kuwa Muislamu?
Allah amefungua milango ya Uislamu kwa wanadamu wote, bila kujali hali zao za zamani au za sasa. Kwa hivyo, mtu yeyote anaweza kuwa Muislamu wakati wowote kwa kuamini tu na kutamka shahada ifuatayo ya imani:
"Nashuhudia kwamba hakuna mungu anayestahili kuabudiwa isipokuwa Allah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah."
Kuwa Muislamu kunamaanisha kutambua ukuu wa Muumba na kujenga na kudumisha uhusiano wa karibu naye kwa kumtii. Hili litaleta furaha na utulivu katika maisha haya na Akhera, na pia kufanikisha lengo la maisha ya mwanadamu.
