Description
Manufaa ya Uislamu
Njia ya Maisha ya Vitendo na sambamba
Uhusiano wa Karibu na wa Moja kwa Moja na Mwenyezi Mungu
dhana Safi na Wazi Kuhusu Mwenyezi Mungu
Ujumbe wa Ulimwenguni na wa Milele
Jifunze Misingi
UISLAMU NI NINI?
Uislamu ni kuamini na kumwabudu Mwenyeazi Mungu Mmoja wa Kweli ("Allah" kwa Kiarabu) peke yake, na kumkubali Mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) kama Mtume Wake wa mwisho.
Takriban mtu moja kati ya watu wanne (23%) ni Muislamu – zaidi ya Waislamu bilioni 1.5.
Wafuasi wa Uislamu wanajulikana kama Waislamu ambao wanaweza kuwa kutoka historia yoyote ya kikabila au rangi.
Imani na msimamo
Mwenyezi Mungu anatuita tumtambue kupitia ishara Zake. Mwenyezi Mungu ameweka kuwa jukumu letu kumtambua. Hii ni sehemu ya mtihani wa maisha haya. Bila mtazamo sahihi, hakuna kiwango cha habari kinachoweza kumfanya mtu kuamini.
Ulinganifu na Akili ya Wazi
Unyenyekevu na ikhlasi
Kutafakari kuhusu lengo letu
Kukubali Ishara za Mwenyezi Mungu
Upendeleo wa awali wa kutoamini
Kiburi na Majivuno
Kuzingatia tu ulimwengu wa kimada
kuangalia kila kitu kama hakina maana
Sababu ya Kwanza: Mwanzo wa Ulimwengu
Sababu ya kwanza ya kumwamini Mwenyezi Mungu inahusiana na kutafakari kuhusu asili ya ulimwengu.
Ulimwengu ulitokeaje?
Je, ulitokea bure? Kutoka kwa chochote, hakuna kinachotokea. Kwa hivyo, hapana.
Je, ulimwengu ulijiumba yenyewe? Hapana, hili ni jambo lisilo la mantiki. Ni kama kusema mama alijifungua mwenyewe.
Je, umekuwepo kila wakati? Hapana, sayansi ya kisasa inabainisha kuwa ulimwengu sio wa milele na una mwanzo.
Je, uliumbwa? Ndio. Waislamu wanaamini kuwa kuna kitu kilicho nje ya ulimwengu kilichoumba - Muumba.
Swali: Lakini nani alimuumba Mwenyezi Mungu?
Jibu: Mungu hakuumbwa. Tofauti na ulimwengu na viumbe vingine, Mungu ni wa milele, yupo daima, na hana mwanzo.
Sababu ya Pili: Mpangilio wa Ulimwengu
Sababu nyingine rahisi ya kumwamini Mwenyezi Mungu ni kutafakari katika mpangilio wa ulimwengu kwa kutumia mantiki ifuatayo:
1. Kila kitu kilichopangwa kinaonyesha akili
2. Mfumo wetu wa jua umewekwa kwa usahihi na mifumo, sheria, na mifumo ya hali ya juu
3. Mpangilio katika ulimwengu wetu unaonyesha akili ya Muumba!
Vipengele vingi vya ulimwengu vinaonyesha wazi kwamba vimeundwa mahsusi kusaidia maisha. Ikiwa vipimo hivi vingekuwa tofauti kidogo na jinsi vilivyo sasa, maisha yasingekuwepo. Mifano iko hapa chini.
Tabaka ya Ozone
Unene wa Ganda la Dunia
Asilimia ya Oksijeni Hewa
Umbali kutoka Jua
Ukubwa wa kiasi maalumu wa Jua, Dunia na Mwezi
Je, ulimwengu mkubwa na mgumu unaweza kuundwa kwa bahati nasibu, bila usimamizi? Inapaswa kuzingatiwa kuwa Uislamu unahimiza utafiti wa kisayansi na kutafakari. Nafasi ya sayansi inatusaidia kuelezea mifumo mingi inayoonekana ambayo Mwenyezi Mungu ameweka katika uumbaji Wake na kuthamini ukubwa wa nguvu na hekima Zake.
Sababu ya tatu
Ufunuo – Qur'an
Qur'an inatoa hoja yenye nguvu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na haina kifani katika mtindo wake, hekima, mwongozo, na ufasha wake katika uzuri wa kuongea na msomaji wa Qur'an .
Hakuna makosa wala migongano
Maelezo safi na wazi ya Mungu
Kilele cha uzuri wa lugha ya Kiarabu
Ilifunuliwa kupitia Mtume Muhammad ambaye hakuwa na elimu ya kusoma na kuandika
Imehifadhiwa na haijabadilika kwa muda wa miaka 1400
Mtazamo wa kina ya tabia ya binadamu
Inahifadhiwa na mamilioni ya watu
Ina maelezo ya kisayansi ya ukweli ambayo hayakujulikana wakati huo
Na katika ardhi kuna ishara kwa wenye yakini; na ndani yenu pia, je, hamuoni? (Qur'an 51:20-21)
Mungu ni nani?
Moja kati ya uzuri mkbwa wa Uislamu ni kwamba unatambua ukamilifu mpana , ukubwa na upekee wa Mwenyezi Mungu bila upungufu wowote.
· Mungu ni Mmoja na wa Pekee na hana mpinzani, mshirika, au mwana.
· Mungu anastahili kuabudiwa pekee na moja kwa moja (bila waombezi)
· Mungu ni Mkamilifu na Hana Kasoro - Hana mipaka wala udhaifu
· Mungu ni Mwenye Huruma Zaidi - Anajua kwamba hatuko wakamilifu na tunatenda madhambi, lakini muhimu ni kutambua makosa yetu kwa dhati na kuomba msamaha kwa kweli.
· Hakuna sehemu ya Mwenyezi Mungu iliyopo katika viumbe vyake wala hakuna anayeshiriki sifa zake za Uungu.
Unapojaribu kuelewa dhana ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu, ni muhimu kujadili hadhi ya Yesu kutokana na mkanganyiko na madai mengi kuhusu asili yake.
Uislamu unatambua Yesu kama Nabii mtukufu na Mtume wa Mwenyezi Mungu, lakini Waislamu hawamwabudu - kwani ibada ni kwa Mwenyezi Mungu pekee ambaye aliumba Yesu na kila kilicho hai. Kwa hivyo, imani kwamba Yesu ni Mungu au mwana wa Mungu au sehemu ya Utatu inapingana waziwazi na mafundisho safi ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu.
Kuna mifano mingi katika mafundisho ya Kikristo ya Yesu akiongea na kutenda kama kwamba Mungu ni kiumbe tofauti naye, mfano Yesu akimwomba Mungu katika swala.
Kama Yesu alikuwa Mungu, alikuwa anafanya ibada kwa nani?
Yesu alizaliwa, akala, akalala, na alikuwa na maarifa ya kikomo - sifa ambazo haziendani na Mungu. Mwenyezi Mungu ana sifa za ukamilifu ilhali mwanadamu ni kinyume chake.
Mungu anawezaje kuwa mkamilifu na asiye mkamilifu kwa wakati mmoja?
Tunapata kwamba neno "mwana wa Mungu" linatumika kwa njia ya kupiga mfano katika lugha za awali za Biblia kwa "mtu mwema" kwa watu wengi - si kwa Yesu peke yake. Mwenyezi Mungu yuko mbali kabisa na kuwa na mwana wa kimwili na halisi.
Neno "mwana wa Mungu" linamaanisha nini hasa?
Swali: Kama Mwenyezi Mungu anaweza kufanya lolote, kwa nini hawezi kuwa mwanadamu?
Jibu: Mwenyezi Mungu daima ana sifa za ukamilifu na hafanyi chochote kinachoweza kupunguza ukamilifu wake. Kwa mtazamo huo Mwenyezi Mungu hafanyi vitendo visivyo vya uungu Kwa hivyo, ikiwa Mungu angekuwa mwanadamu na amepata sifa za wanadamu,kwa hakika asingekuwa Mungu tena.
Manabii wengi
Nabii Adam
Nabii Nuhu
Nabii Ibrahimu
Nabii Musa
Nabii Yesu
Nabii Muhammad
MANABII WENGINE
Amani iwe juu yao wote
Dhamira Moja
• Kusisitiza dhana ya Mungu Mmoja
• Kukataa miungu ya uongo na imani potofu
• Kuonyesha jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu
• Kuwa mfano wa kuigwa
• Kuelezea thawabu za utiifu (peponi)
• Kuonya kuhusu adhabu ya kufanya maasi (motoni)
Mungu alituma manabii kwa kila umma katika zama zote wakati wote na ujumbe ule ule wa msingi. Ingawa Waislamu wanawapenda na kuwaheshimu manabii wote, lakini hawawaabudu wala kuwapa sifa za uungu, kwani hili limetengwa kwa Mwenyezi Mungu pekee.
lengo la Maisha
Mwenyezi Mungu, Mwenye Hekima, hakutuumba ili tuishi bila lengo au kutimiza tu matamanio na hisia zetu za msingi. bali, tuna lengo la juu zaidi – ni kumtambua na kumwabudu Mungu pekee.ili tuweze kuishi kulingana na mwongozo wa muumbaji wetu
Mwongozo huu hutuwezesha kuishi maisha yenye mafanikio na kuridhika katika Nyanja zote.
Ni sehemu ya hekima ya Mwenyezi Mungu isiyo na mipaka ya kwamba alituumba na kutupa nafasi ya kujua nafsi zetu, kuishi maisha yetu, na kufanya maamuzi yetu wenyewe.
Uislamu ni njia kamili ya maisha na ya vitendo inayofundisha Waislamu kuwa watu wenye usawa, wenye tabia njema, na wanaochangia katika jamii.
Dhana ya ibada katika Uislamu haijumuishi tu kusali na kuomba kwa Mwenyezi Mungu.bali Ni ufafanuzi mpana unaojumuisha kitendo chochote ambacho Mwenyezi Mungu anaridhika nacho. Na mifano hapo chini
· Kupata riziki kwa njia ya halali
· Kupinga dhuluma
· Kuwatunza mayatima
· Kutunza mazingira
· Kuwa na subira na unyenyekevu
· Kuleta faida kwa jamii
· Kuheshimu wazazi
· Kusimama kwa ajili ya haki
· Kuwatendea wema majirani
· Kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumcha
· Kuwasaidia familia mahitaji yao
· Kusema ukweli
Matendo ya ibada yanahitaji nia ya kweli ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu na kufanywa kwa usahihi kulingana na mafundisho ya kiislamu.
UISLAMU UNASEMA NINI KUHUSU...
· Wanawake: Wanawake wana hadhi kubwa ya heshima katika Uislamu. Wanapaswa kutendewa kwa upendo, heshima, na ukarimu. Ni washirika wa wanaume, na dhuluma haiwezi kamwe kuhalalishwa dhidi yao.
· Ugaidi: Uislamu unaruhusu kupigana ili kuhifadhi ustawi wa jamii, kuzuia dhuluma, na kukuza uadilifu. Hata hivyo, kulenga wasio na hatia ambao si wapiganaji ni kitendo cha kuchukiza na kinakatazwa.
· Chakula Halali: Vyakula vya halali ni vile vinavyoruhusiwa kwa Waislamu kula. Nyama na kuku wanapaswa kuchinjwa kwa ubinadamu huku mateso yakiwa yamepunguzwa, na jina la Mwenyezi Mungu litajwe wakati wa kuchinja.
· Mageuzi: Mungu aliumba mwanadamu wa kwanza, Adam, katika umbo lake la mwisho - kinyume na kuendelea polepole kutoka kwa sokwe walioendelea. Hili haliwezi kuthibitishwa au kupingwa moja kwa moja na sayansi kwa sababu lilikuwa tukio la kipekee na la kihistoria - muujiza. Kuhusu viumbe hai wengine isipokuwa wanadamu, vyanzo vya Kiislamu havizungumzii jambo hilo na vinahitaji tu tuamini kuwa Mwenyezi Mungu aliwaumba kwa njia yoyote aliyoitaka, akitumia mageuzi au vinginevyo.
Mtazamo wa Muislamu kuhusu Maisha
Nina lengo tukufu
Kuweka uwiano kati ya tumaini katika Rehema za Mwenyezi Mungu na hofu ya adhabu Yake
Ikiwa jambo jema linatokea, shukuru. Ikiwa jambo baya linatokea, vumilia
Imani yangu upo kwa Mwenyezi Mungu – Hakuna kinachotokea isipokuwa kwa idhini Yake
Maisha haya ni mtihani na Mwenyezi Mungu anaona kila kitu ninachofanya
Kila kitu nilicho nacho kimetoka kwa Mungu Mwenyezi
Nilenge kile kilicho chini ya uwezo wangu na nijitahidi kadri ya uwezo wangu
Tumaini na wasiwasi wa kweli kwa kuwaelekeza wasio Waislamu waongozwe
Nitarudi kwa Mwenyezi Mungu na nitalipwa
