Haki za Wanawake Katika Uislamu حقوق المرأة فى الإسلام

3.85 MB 108 1 Files
albyan
or download free
[free_download_btn]

Description

anaheshimiwa. .anakirimiwa. anathaminiwa.

Utangulizi

Wanawake katika Uislamu wanadhaniwa kuwa wametiishwa, wamepuuzwa, na wameonewa - lakini je, ni kweli? Je, mamilioni ya Waislamu ni wenye ukandamizaji kama huo au hizi dhana potofu zimeundwa na vyombo vya habari vyenye upendeleo?

"Na wanawake wana haki juu ya wanaume, sawa na zile za wanaume juu yao." (Qur'ani 2:228)

Zaidi ya miaka elfu moja na mia nne iliyopita, Uislamu uliwapa wanawake haki ambazo wanawake wa Magharibi hawakuanza kuzifurahia isipokuwa hivi karibuni tu. Katika miaka ya 1930, Annie Besant aliona, " Uingereza wa Kikristo haikutambua haki ya mwanamke kwenye kumiliki mali isipokuwa katika miaka ishirini iliyopita tu, wakati Uislamu umeiruhusu haki hii tangu mwanzo." "Ni uongo kusema kwamba Uislamu unafundisha kwamba wanawake hawana roho." (Maisha na Mafundisho ya Muhammad, 1932)

Wanaume na wanawake wote walitokana na mtu mmoja - Nabii Adam (amani iwe juu yake). Uislamu haukubali lolote kwa yeyote kati yao isipokuwa haki na matendo mema.

Malipo ya Sawa na Uwajibikaji wa Sawa

Wanaume na wanawake wanamwabudu Mwenyezi Mungu kwa njia ile ile, wakimaanisha kwamba wanamwabudu Mungu mmoja (Allah), wanatekeleza ibada ile ile, wanafuata kitabu kimaoja kitakatifu, na wana imani moja. Allah (neno la Kiarabu kwa Mungu mmoja wa kweli wa viumbe vyote), anahukumu wanadamu wote kwa haki na usawa. Allah anasisitiza uadilifu katika aya nyingi za Qur'ani na malipo yanayostahili wanaume na wanawake:

"Allah amewaahidi Waumini, wanaume na wanawake, mabustani ambayo mito inapita chini yake, na majumba mazuri katika mabustani ya neema ya milele." (Qur'ani 9:72)

"Sitamruhusu kazi ya mfanyakazi yeyote kati yenu, mwanaume au mwanamke, kupotea; nyote ni wa kila mmoja." (Qur'ani 3:195)

Aya hizi zinaonyesha kuwa malipo yanategemea matendo ya mtu na si jinsia yake. Jinsia haina nafasi yoyote katika jinsi mtu anavyolipwa na kuhukumiwa.

Tukilinganisha Uislamu na dini zingine, tunaona kuwa inaweka uadilifu kati ya jinsia mbili. Kwa mfano, Uislamu unakataa wazo kwamba Hawa analaumiwa zaidi kuliko Adam kwa kula kutoka kwa mti ulioharamishwa. Kulingana na Uislamu, Adam na Hawa wote walikosea, wote walitubu na Mungu akawasamehe wote wawili.

Haki ya sawa Sawa ya Kujifunza

Wanaume na wanawake wanahimizwa kwa usawa kutafuta elimu. Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) alisema, "kutafuta Elimu ni wajibu kwa kila Muislamu."

Pia, walikuwepo wanazuoni wakubwa wa Kiislamu wa kike katika zama ya Mtume na mazingira yake (rehma na amani ziwe juu yake). Wengine walitoka kwa familia yake na wengine walikuwa masahaba wake au mabinti zao. Maarufu miongoni mwao alikuwa Aisha, mke wa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake), ambaye kupitia yeye robo ya sheria ya Kiislamu ilihamishwa.

Wanawake wengine walikuwa wanazuoni wakubwa wa sheria za Kiislamu na walikuwa na wanafunzi wa kiume maarufu.

Haki ya sawa Sawa ya Kuchagua Mwenza

Uislamu umewaheshimu wanawake kwa kuwapa haki ya kuchagua mwenza na kuhifadhi jina la familia yao ya asili baada ya ndoa. Aidha, wengi wana maoni kwamba wazazi wanawalazimisha binti zao kuolewa.

Hii ni desturi ya kitamaduni, na haina msingi wowote katika Uislamu. Kwa kweli, imekatazwa.

Wakati wa Mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake), mwanamke mmoja alimjia na kusema, "Baba yangu ameniozesha kwa binamu yangu ili kuinua hadhi yake ya kijamii, na nililazimishwa kufanya hivyo." Mtume alimtuma baba wa msichana, kisha mbele yake alimpa msichana chaguo la kubaki kwenye ndoa au kubatilisha ndoa hiyo. Akamjibu, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimekubali alichofanya baba yangu, lakini nilitaka kuwaonyesha wanawake wengine (kwamba hawawezi kulazimishwa kuolewa)."

Wako Sawa sawa Lakini wameTofautiana

Ingawa wanaume na wanawake wana haki sawa sawa kama ni kanuni ya jumla, haki na majukumu maalum waliyopewa si sawa. Wanaume na wanawake wana haki na majukumu yanayokamilishana.

Tukiachana na tofauti za nje na za ndani za anatomia, wanasayansi wanajua kuwa kuna tofauti nyingi za kina katika namana ambyo akili za wanaume na wanawake zinavyosindika lugha, taarifa na hisia, kwa mfano.

Mtaalamu wa biolojia ya kijamii, Edward O. Wilson wa Chuo Kikuu cha Harvard, alisema kwamba wanawake wana mwelekeo wa kuwa juu zaidi ya wanaume katika ujuzi wa maneno, huruma, na ujuzi wa kijamii, kati ya mambo mengine, wakati wanaume wana mwelekeo wa kuwa juu katika uhuru, kutawala, ujuzi wa sehemu na hesabu, uchokozi unaohusiana na cheo, na sifa nyingine.

Ingekuwa ni upumbavu kuwatendea jinsia zote kwa njia ile ile na kupuuza tofauti zao. Uislamu unafundisha kwamba wanaume na wanawake wana majukumu yanayokamilishana, lakini inatofauti, kwa sababu yanafaa zaidi kwa asili yao. Mwenyezi mungu anasema:

"Na mwanamume si kama mwanamke." (Qur'ani 3:36)

"Je, yule aliyeumba hajui? Na Yeye ndiye Mpole, Mwenye Kujua." (Qur'ani 67:14)

Kitengo cha Familia

Mungu aliwaumba wanaume na wanawake kuwa tofauti, wakiwa na majukumu, ujuzi na wajibu wa kipekee. Tofauti hizi hazionekani kama ushahidi wa ubora au uduni, bali wa utaalamu. Katika Uislamu, familia ni msingi wa umuhimu Mwanaume anawajibika kwa ufadhili wa kifedha wa familia huku mwanamke akichangia ustawi wa kimwili, kielimu na kihisia kwa familia. Hii inahimiza ushirikiano badala ya ushindani. Kwa kutimiza majukumu yao ya pamoja, familia inajengeka imara na hivyo hivyo jamii inakuwa imara.

Pia, kihisia, wanaume na wanawake hawaishi maisha yenye furaha bila ya kuishi pamoja . Mwenyezi Mungu anaelezea hili kwa uzuri akisema:

"Wao ni vazi kwenu na ninyi ni vazi kwao." (Qur'ani 2:187)

Mavazi yanatoa faraja, joto na usalama pamoja na kufanya mtu aonekane vizuri – hivi ndivyo uhusiano kati ya mume na mke unavyofafanuliwa katika Uislamu.

Upendo na Huruma Katika Mahusiano ya Ndoa

Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) pia aliwatia moyo wanaume kuwatendea wake zao kwa njia bora, "Mbora wenu ni wale walio bora kwa wake zao."

"Na miongoni mwa Ishara Zake ni kuwa Amekuumbeni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao; na Ameweka mapenzi na huruma kati yenu. Hakika katika hayo Ishara kwa watu wanaotafakari." (Qur'ani 30:21)

Aisha (mke wa Mtume) aliulizwa mara moja kuhusu mwenendo wa Mtume nyumbani kwake. Akasema: "Alikuwa kama mmoja wenu nyumbani, lakini alikuwa mpole zaidi na mkarimu zaidi... Alikuwa tayari kusaidia wake zake katika kazi za kawaida za nyumbani, alishona nguo zake mwenyewe na kurekebisha viatu vyake." Kwa ujumla, alisaidia katika kazi yoyote ambayo wake zake walifanya.

Nafasi za Juu za Mama na Mabinti

Mama ana ushawishi mkubwa zaidi kwa mtoto, hasa katika miaka ya awali kupitia upendo wake, huruma na mapenzi. Bila shaka, mafanikio ya jamii yanatokana na mama. Kwa hivyo, ni sawa kwa Uislamu kuwaheshimu na kuinua hadhi yao.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'ani:

"Na tumemwusia mwanadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Mama yake alimchukua kwa taabu na alimzaa kwa taabu." (Qur'ani 46:15)

Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) aliulizwa mara moja, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nani anayestahili zaidi kupewa wema wangu?" Akasema: "Mama yako." Mtu huyo akauliza mara mbili zaidi, "Halafu nani?" na akapewa jibu lilelile. Hadi mara ya nne ndipo Mtume alijibu: "Halafu baba yako."

Malipo mema haitolewi tu kwa wema na ukarimu kwa mama. Kwa kweli, Uislamu umeweka tuzo maalum kwa kulea mabinti ambayo haitolewi kwa kulea watoto wa kiume.

Mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) alisema: "Yeyote ambaye Mwenyezi Mungu amempa mabinti wawili na alikuwa mwema kwao, watakuwa sababu ya yeye kuingia Peponi."

Hitimisho

Kabla ya Uislamu, wanawake walichukuliwa kuwa fedheha, watoto wa kike walizikwa wakiwa hai, ukahaba ulikuwa umeenea, talaka ilikuwa mikononi mwa mume pekee, urithi ulikuwa kwa wenye nguvu tu, na dhuluma ilikuwa imeenea. Uislamu ulifika na kukomesha mazoea haya.

Hata sasa, katika "nchi zilizoendelea", wanawake hawapewi heshima, hadhi na utukufu,pamoja na malipo sawa kwa kazi sawa. Hata hivyo, Uislamu unawaona wanawake kuwa ni hazina kubwa na wa thamani, hawapaswi kudharauliwa au kudhalilishwa. Unyanyasaji wa wanawake katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati au familia za Waislamu unasababishwa na sababu za kitamaduni ambazo baadhi ya Waislamu hufuata vibaya, si kwa sababu ya Uislamu. Kwa nini wanawake wengi ulimwenguni wajiunge na Uislamu kwa hiari ikiwa ni dini ya ukandamizaji?

Tunamalizia kwa maneno ya Mola wetu na Mola wenu, Muumba na Mlezi wa wanaume na wanawake wote:

"Hakika Waislamu wa kiume na wa kike, na waumini wa kiume na wa kike, na watiifu wa kiume na wa kike, na wakweli wa kiume na wa kike, na wavumilivu wa kiume na wa kike, na wanyenyekevu wa kiume na wa kike... Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na thawabu kubwa." (Qur'ani 33:35)

Similar Downloads

No related download found!